Wana michezo wa UMITASHUMTA waliochaguliwa kutoka kanda ya Kasanda na Kakonko wakiwa wanasubiri kuungana na wana michezo kutoka kanda ya Nyaronga ili kuunda timu ya Wilaya wahehimziwa kuendelea kufanya mazoezi ziaidi ili kuiwakilisha Wilaya ya Kakonko katika mashindano ambayo yatafanyika ngazi ya mkoa hivi karibuni.
Wakazi wa Kijiji cha Nyamtukuza Kata ya Nyamtukuza kilichopo tarafa ya Nyaronga wameeleza kuwa kukosekana kwa soko kumewasababishia adha mbalimbali ikiwemo kunyeshewa na mvua wanapokuwa wakipata mahitaji yao eneo la soko.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Kakonko kupitia program ya TAKURURU rafiki imeanza kutatua kero za Wananchi ikiwemo kero ya maji katika kata tatu za Kanyonza, Gwarama na Nyamtukuza kati ya kata 13 zilizopo.
HatimilikiĀ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Haki zote zimehifadhiwa